Jumapili, 12 Februari 2017

Mkulima mmoja wa kichina chini ya ulinzi

Mkulima mmoja wa Kichina ameishtaki kampuni kubwa ya kemikali iliyotengeneza kemikali za sumu zilizoharibu mashamba ya wakulima. Mahakama sasa imeamuru wakulima walipwe fidia ya Euro 110,000. Cha kushangaza ni kwamba mkulima aliyefungua mashtaka amesoma mpaka darasa la tatu tu na aliamua kwenda kwenye duka la kuuza vitabu na kusoma vitabu vya sheria kwa miaka kumi ili kuweza kufungua kesi mahakamani. Kisa hiki kinaonyesha kwamba kila kitu kinawezekana ukifanya juhudi. Tunakutakia wikiendi njema!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni