Kijugu: jiandaeni kufanya mubashara
MSIMAMIZI wa vipindi vya radio wa chuo cha Rpyal, RCT, Samuel kijugu amesema
mubashara utaendelea kuwepo pindi umeme ukikatika chuoni hapo.
Awali kurikuwa na utaratibu wa kupendekeza maada ambayo imeandaliwa na darasa
husika na kujadiliwa na wanafunzi wote pindi ambapo kunakuwepo na ukosefu wa umeme
chuoni hapo.
Kijugu alisema hayo wakati akizungumza na wanafunzi katika ukumbi wa kamongo jana,
na kubainisha kuwa kwa sasa vipindi vya radio vitakuwa vikiruka hata kama hakuna
umeme hivyo amewataka wanafunzi kuwa tayari na kuacha mazoea ya kuandaa maada
pindi ambapo kuna tatizo la umeme.
“napenda mubashara iwepo ili kuimalisha ufanishi na ujasili wa wanafunzi katika kufanya
vipindi n ahata uwasilishaji wake kwani kupitia mubashara wanafunzi watakuwa na
confidence ya kusimama mbele za watu sehemu yoyote ile,”alisema na kuongeza kuwa ni
lazima wanafunzi wote wa kitivo cha habari kuwa na ujasili wa kusimama mele za watu na
kuwasilisha kipindi chake.
Aidha kijugu aliwapongeza wanafunzi wa kitivo cha uandishi wa mhula wa septemba kwa
kurusha vipindi vyao mubashara na kuwataka wanafunzi wengine kuiga mfano huo
“huu ni ubunifu mkubwa ambao wenzenu wameuonyesha kama wanafunzi ni lazima
kuinga ufanyaji wa vipindi live kama wenzenu walivyofanya leo hapa,” alisema kijugu.
Mbali na hayo kijugu aliwataka wanafunzi kuendelea kufuata sharia na taratibu ikiwa
pamoja na kuwasilisha habari mapema kwaajili ya kupitiwa na kurekebishwa makossa
mapema kabla ya muda wa kufanya Makala ya wanafunzi kufika.
“napenda kusisitiza na kuwakumbusha wanafunzi kuleta habari zao kwa wakati ili kupitiwa
na kurekebishwa makossa mapema, hii itawapa nafasi ya kufanya marekebisho mapema,”
alisema kijigu.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi ambao walishiriki katika ufanyaji wa vi[pindi
mubashara, Diana Morsad, alisema kufanya vipindi mubashara imewapa ujasili mkubwa
ikiwa pamoja na kuongeza umakini pindi wanapokuwa wakiwasilisha vipindi vyao.
“yaanii kufanya vipindi live kumenipa ujasili sana kwani nilikuwa naogopa sana kufanya
kipindi changu, ila kwa sasa sin ahata hofu naweza kusimama sehemu yoyote na kuwasilisha
kipindi changu bila uoga,” alisema Morsad.
Aidha Morsad aliwataka wanafunzi wengine kuinga mfano huo kwani unawapa ujasili
wa kusimama mbele za watu na kuwasilisha ki[pindi .
Morsad alisema kupitia ufanyaji wa vipindi mubashara itasaidia kuongeza ufanisi wa
vipindi vya radio na kupunguza makossa ambayo yaliyokuwa yakifanyika hapo awali
kwa wanafunzi kukosa ujasili hali inayopelekea kufanya vipindi vyenye mapungufu
makubwa.
“tukifanya hivi mara mbili naamini kutakuwa na mabadiliki makubwa kwenye ufanyaji
wetu wa vipindi na kuachana na kuwa na vipindi vibovo.”alisema Morsad
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni